Kwanza kabisa tunatakiwa kujua, Paulo alimaanisha nini alipotamka maneno haya; sheria, dhambi, neema, imani, haki, mwili na roho. Bila hivyo...
Kwanza kabisa tunatakiwa kujua, Paulo alimaanisha nini alipotamka maneno haya; sheria, dhambi, neema, imani, haki, mwili na roho. Bila hivyo hakuna faida kusoma barua zake.
Hautakiwi kuelewa neno “sheria” kwa jinsi ya kibinaadamu, kwa mfano; urekebishaji wa matendo gani yanatakiwa kufanywa au hayatakiwi. Hii ni jinsi ya sheria ya kibinaadamu; kwamba unafanyia kazi sheria hata kama moyo wako unataka au hautaki. Mungu huhukumu kilicho ndani ya moyo. Hivyo basi sheria yake hutaka moyo uitimize, na haiuachi uridhie kuitenda; badala yake inaadhibu kama unafiki na uongo matendo yote yaliyofanywa na mwili mbali na moyo. Ndiyo maana wanadamu wote wameitwa waongo (Zaburi 116:11) tangu pale hakuna hata mmoja anayetunza sheria ya MUNGU kutoka ndani ya moyo. Kila mtu ataona ndani yake mwenyewe, kuna chuki ya mema na tamaa ya mabaya. Hapo moyo hauko tayari kwa ajiri ya sheria ya MUNGU, na hapo ndipo dhambi ilipo na kustahili hasira kali ya Mungu, hata kama kwa nje ulionekana na matendo mema, na maisha yenye heshima kwa watu kiasi gani.
Warumi 2:13 Paulo akasema, “Wayahudi wote ni wenye dhambi.” Akaendele kusema, “Watendaji wa sheria pekee ndio wenye haki mbele za Mungu.” Alichomaanisha ni hivi, “hakuna hata mmoja ambaye ni mtendaji wa sheria kwa kuifanyia kazi.”
Katika Warumi 2:21 akawaambia, “Mwafundisha mtu asizini hali ninyi mwazini.” “Mwahukumu mtu kwa jambo flani na kujiadhibu wenyewe kwa jambo hilo hilo, maana mwafanya kile kile mnachomhukumu mwingine; ni kama alisema, “Kwa nje mnaishi sawa kabisa kwa kufanyia kazi sheria, na kuwahukumu wale wasioenenda kama ninyi.
Kwa nje mnatunza sheria kwa kuifanyia kazi, bila kuipenda wala hofu ya hukumu. Ni kana kwamba mnafanya kila kitu, bila nia huru na upendo wa sheria; mnatenda sheria kwa chuki na kujilazimisha. Na kama sheria haingelikuwepo mngetenda hayo hayo inayoyakataza.
Akaendelea kusema, ndani ya mioyo yenu ni maadui wa sheria. Nini mnachomaanisha kwa kufundisha mwingine asiibe, ambapo ninyi ni wizi ndani ya mioyo yenu? mwaweza kuwa hata kwa nje pia (maana matendo ya nje hayachukui mda mrefu kwa unafiki kama huo.) Hivyo, mnafundisha mwingine na sio ninyi wenyewe; Hamjui hata mnachokifundisha, kamwe hamjaielewa sheria vizuri. Zaidi sana sheria huongeza dhambi, kama Paulo alivyosema katika Warumi 5:20 kwamba, ni kwasababu mtu huwa zaidi na zaidi adui wa sheria kadri inavyotaka kile asichoweza kufanya.
Warumi 7:14 Paulo akasema, “sheria ni ya kiroho.” Je hapo alimaanisha nini? Kama sheria ingekuwa ya kimwili ingetimizwa kwa kuifanyia kazi, lakini kwa sababu ni ya kiroho hakuna hata mmoja anayeweza kuitimiza mpaka kila anachofanya kitoke moyoni. Lakini hakuna hata mmoja awezaye kutoa moyo kama huo isipokuwa ni ROHO WA MUNGU amfanyae mtu kuwa kama sheria, humjengea mtu tamaa ya moyo wa dhati kwa ajiri ya sheria na kufanya kila kitu, bila woga na chuki bali kwa moyo huru. Sheria kama hiyo ni ya kiroho tangu pale inapopendeka na kutimizwa na moyo ulio na ROHO WA MUNGU. Kama ROHO hayupo kwenye moyo kinachobaki pale ni dhambi, chuki na uadui wa sheria.
Matendo ya sheria ni kitu ambacho unaweza kufanya kwa kutaka mwenyewe, lakini kwa sababu wakati unafanya hivyo moyo unachukia na unaulazimisha kutii, matendo yote uliyofanya kwa nje yanakuwa ni hasara.
Hicho ndicho Paulo alimaanisha aliposema, “hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki…kwa matendo ya sheria…” Warumi 3:20
Kutokana na hayo unaweza kuona kwamba, walimu wa kanisa la roma ni waongo wanapofundisha kuwa, “unaweza kujiandaa kwa ajiri ya neema kwa matendo.”
Vipi mtu yeyote ajiandae kwa ajiri ya mema kwa matendo, ikiwa hafanyi matendo mema ispokuwa pamoja na chuki, na vikwazo moyoni?
Vipi matendo hayo yampendeze Mungu, ikiwa yanatoka katika moyo usiotaka na wenye chuki?
Lakini kutimiza sheria ni kuifanya kwa bidii, upendo na uhuru, bila kukwazika moyoni; ni kuishi kwa kumpendeza Mungu, fikiri kama vile hakuna sheria wala hukumu (Wagaratia 5:2)
Kwa vyovyote, ni Roho Mtakatifu ambaye huweka bidii yenye upendo kama huo moyoni. Lakini Roho huja kwa imani ya Yesu, na imani huja kwa neno la Mungu, Injiri inayomhubiri Kristo; jinsi gani ni Mwana wa Mungu na mtu, alikufaje na kufufuka kwa ajiri yetu.
Hii ndiyo sababu imani pekee humfanya mtu mwenye haki na kutimiza sheria; imani huleta Roho Mtakatifu, Roho kwakubadilika huufanya moyo huru na wenye furaha kama sheria inavyotaka. Ndipo matendo mema yanaendelea kutokana na imani pekee. Paulo alimaanisha hivyo katika Warumi 3:28 alipotaka kutupia mbali matendo ya sheria, alikuwa kama anataka kutangua sheria kwa sababu ya imani. Hapana alisema, “tunatimiza sheria kwa njia ya imani” (Rum 3:31.)
Hakuna dhambi iliyowahi kufanywa kwa nje tu mpaka mtu aitende katika mwili na roho. Hasa Maandiko huangalia moyo kwenye mzizi wa dhambi zote. Kama imani pekee huleta haki, Roho na tamaa ya kufanya mema kwa nje, hivyo ni wasioamini tu ndiyo hufanya dhambi na kusifu mwili na kuleta tamaa ya kufanya uovu kwa nje. Ndiyo maana wasioamini Kristo Aliwaita “wenye dhambi” aliposema, “Roho atauhakisha ulimwengu…kwa habari ya dhambi kwa sababu hawaniamini mimi.” Yohana 16:8-9.
Neema ni huruma au wema wa Mungu ambao kwa huo amemtoa Kristo na Roho pamoja na kalama kwa ajiri yetu, kama Paulo alivyosema “…kwa yeye (Kristo) tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema hii…” Warumi 5:2
Kalama na Roho huongezeka ndani yetu; maana havijakamilika, kwa sababu ya tamaa mbaya na dhambi zilizobaki ndani yetu zinazopigana vita na Roho, kama Paulo alivyosema katika Warumi 7:23 na Wagalatia 5:17
Neema ya Mungu hufanya yote haya kwamba, tunahesabiwa haki kikamilifu mbele za Mungu.
Neema haijagawanyika kama zilivyo kalama, lakini neema hutuchukua kikamilifu kuwa wana wa Mungu kupitia Kristo mpatanishi wetu, ndipo karama zinaanza kazi ndani yetu.
Kwa njia hii utaelewa Warumi 7 Paulo anaposema, yeye mwenyewe bado ni mwenye dhambi.
Warumi 8:1 Paulo akasema, “kwa sababu ya karama ambazo hazijakamilika, na kwa sababu ya Roho, Hakuna laana kwa walio katika Kristo,” kwa sababu miili yetu haijafa, bado tu wenye dhambi, lakini kwa sababu tunamwamini Kristo na tumeanza kuwa na Roho, Mungu anatuonyesha wema na huruma yake, kwamba haangali, wala hahukumu dhambi kama hizo, badala yake anashugulika nasi kutokana na imani yetu katika Kristo mpaka dhambi itakapokufa.
Imani sio ndoto au maono ya kibinaadamu kama baadhi wanavyodhani.
Wengi wanaodai kuwa wana imani lakini hawana matendo mema yanayotokana na imani, ni kwa sababu, wanaposikia Injili, hujenga wazo moyoni kwa nguvu zao wenyewe na kusema “naamini” wazo hili wanalichukulia kama imani ya kweli. Lakini kwasababu ni ujengefu wa wazo la kibinaadamu inakuwa ni bure.
Imani ni kazi ya Mungu ndani yetu, ambayo hutufanya tuzaliwe upya na Mungu (Yohana 1:12)
Humuua Adam wa zamani na kutufanya tofauti katika moyo, mawazo, akili na nguvu zetu zote, na kuleta Roho Mtakatifu.
Kitu kilicho hai chenye nguvu ni imani; haiwezekani kwamba, imani isimamishe matendo mema, lakini humwendesha mtu kufanya matendo mema.
Imani siku zote ni tendaji. Yeyote asiefanya hivyo hana imani.
Imani ni ujasiri usiotikisika katika neema ya Mungu; ni hakika kwamba, kupitia imani mtu anaweza kufa mara elfu. Kuamini kwa aina hii na kufahamu neema ya Mungu, humfanya mtu kuwa mwenye furaha, ujasiri na kumheshimu Mungu na viumbe vyote. Kupitia imani mtu huwa hana dhambi na mwenye bidii katika AMRI za MUNGU. Kwa njia hii humheshimu Mungu na kufanya mapenzi yake. Hiki ndicho Roho hufanya kupitia imani, hivyo chochote kilicho nje na imani ni dhambi, unafiki na uongo.
Kama isivyowezekana kutoa mwanga katika moto uwakao, pia haiwezekani kutoa matendo kwenye imani.
Hivyo kuwa makini juu ya wapayukaji wanaodhani wanaakili za kutosha, kutoa hukumu juu ya imani na matendo mema. Muombe Mungu afanye imani ndani yako (Yohana 6:44, 65) Vinginevyo utabaki kwa ndani bila imani, hata kama mawazoni umejaribu kuijenga kiasi gani.
Mtu wa “Kiroho” ni yule ambaye matendo yake ya nje ni kama ya Kristo; mfano, alipoosha miguu ya wanafunzi wake. Tena mtu ni wa “kimwili” ambaye ndani na nje, huishi akifanya mambo yenye faida mwilini, na ya mda tu.
Mtu ni wa “kiRoho” ambaye nje na ndani, huishi akifanya mambo yenye faida Rohoni, na katika maisha yajayo.

COMMENTS