Mwarobaini ni mti maarufu sana na unajulikana karibu kila mahali. icha ya kujulikana kila mahali mti huu una kivuli mwanana. Lakini jina h...
Mwarobaini ni mti maarufu sana na unajulikana karibu kila
mahali. icha ya kujulikana kila mahali mti huu una kivuli mwanana. Lakini jina
hili la mti huo limetokana na uwezo wake wa kutibu zaidi ya magonjwa arobaini.
Ingawaje mti huu si majani wala mizizi ni mchungu mno kwa mtumiaji.
Lakini inasadikia kuwa mti huu asili yake imetokea nchini ondoa,
na pia ina uwezo mkubwa wa kustawi sehemu zenye ukame zaidi. Kwa
hapa Tanzania ukienda maeneo ya Dodoma utakubaliana na ukweli huu.
Labda tuangazie macho japo kwa uchache kwa kuona maajabu ya mti huu kama
ifuatavyo.
1. Mwarobaini ni dawa ya kuua minyoo yote tumboni,
2. Hutubu homa, hasa zile homa za usiku
3. Mwarobaini hutibu kikohozi.
4. Mwili kuwaka moto.
5.kuharisha pamoja na tatizo la vidonda vya tumbo. Chukua majani ya mmea
huu kisha yatafune bila kujali uchungu
yaliyo nayo.
6.Mwarobaini hutubu matatizo ya macho.
Ili kutibu matatizo ya macho Unachotakiwa kufanya ni kufuata maelekezo
kama amabayo nitaeleza hapo chini.
7.magonjwa mbalimbali ya ngozi hutibika pia kwa kutumia mti huu wa
mwarobaini.
Kwa kutibu magonjwa hayo na magonjwa mengineyo unachotakiwa kufanya:
Chemsha majani 40 ya mti wa mwarobaini kwa muda wa dakika kumi tano,
baadae acha mchanganyiko huo upoe, kisha chuja kwa ajili ya matumizi.
Unaweza ukanywa mchanganyiko huu asubuhi na jioni. Kwa kiwango cha kikombe
kimoja cha chai. Kikombe kimoja asubuhi na kingine jioni.
COMMENTS